KINGAZI BLOG

KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Latest Post

Friday, 24 March 2017

VIDEO: Rais Magufuli Katoa ONYO Kwa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Wakati akiwaapisha Dr Harrison Mwakyembe na Prof Palamagamba Kabudi, Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John P. Magufuli, leo amewaapisha Dr Harrison Mwakyembe na Prof Palamagamba Kabudi pamoja na mabalozi kadhaa Ikulu Jijini Dar.

Mwakyembe ameapishwa kuwa Waziri mpya wa habari, Profesa Kabudi kaapishwa kaapishwa kuwa waziri wa Katiba na Sheria.

==>Haya ni mambo machache aliyoyasema Rais Magufuli Leo

1.Kuna wengine walisema Kinana leo angezungumza na waandishi, wakati nimemtuma India ambapo atakuwa kwa zaidi ya siku 10

2.Tunataka kuitoa nchi katika hali ya mazoea kuipeleka katika mstari ambao ni sahihi

3.Ukiangalia siku iliyofuata baada ya Rais wa Benki ya Dunia kuja, magazeti yote yaliandika habari nyingine tofauti-

4.Niwatake waandishi wa habari muwe wazalendo, Tanzania ikiharibika na nyie pamoja na wanaowatuma muandike wote mtaharibikiwa

5.Hata magazeti ya leo yana picha ya mtu mmoja ambaye amefanya kosa moja, utadhani kosa ni linaungwa mkono na serikali

6.Niwatake wamiliki wa vyombo vya habari muwe waangalifu, kama mnadhani mna uhuru wa namna hiyo, kuweni makini sana

7.Kuna vyombo vingine vya habari sehemu yenye ugomvi ndio wanapeleka kamera na habari hizo zinapewa muda mrefu, 'watch out'

8.Vyombo vingine haviandiki mazuri ya mtu, lakini wakipata mabaya yake ndiyo yanajaza kurasa

==>Tazama hii Video kumsikiliza Rais Magufuli akiongea Pamoja na walichoongea wateule wa Rais


 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya March 24

Umeipata hii!! Tanzania kuanzisha Kiwanda cha kutengeneza Mabasi.


Balozi wa Hungary hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi, Kenya Mhe. Lazaro Eduard Mathe amemhakikishia Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli kuwa nchi yake ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza sekta ya viwanda

Pia Balozi huyo amemuhakikishia kwamba wawekezaji kutoka Hungary wameanza kufanya mchakato wa kujenga kiwanda cha kuunda mabasi ya abiria.

Mhe. Lazaro Eduard Mathe amesema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na Mhe. Rais Magufuli muda mfupi baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho akiwa ni miongoni mwa Mabalozi sita waliokabidhi hati hizo.

Pamoja na nia ya kujenga kiwanda cha kuunda mabasi ya abiria, Mhe. Lazaro Eduard Mathe amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa juhudi kubwa anazofanya kujenga uchumi wa Tanzania na ameahidi kuwa Hungary itakuza na kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania kwa kuleta teknolojia katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda na kilimo pamoja na kuwahimiza wawekezaji kuja kuwekeza nchini Tanzania.

Thursday, 23 March 2017

POLISI WAZUIA MKUTANO WA NAPE NA WAANDISHI WA HABARI....ALAZIMIKA KUONGEA AKIWA KWENYE GARI LAKE

Aliyekuwa Waziri wa Habari,  Nape Nnauye amezungumza na Waandishi wa habari akiwa juu ya gari lake leo maeneo ya St. Peter Osterbay Dar es salaam  ikiwa ni saa chache kabla ya taarifa kutoka IKULU kutangaza kwamba uteuzi wake umetenguliwa.

Hali hiyo imetokana na Jeshi la Polisi kuuzuia mkutano huo ambapo RPC Kinondoni alifunga barabara kwa gari kuzuia Gari ya Nape huku akiwataka waandishi wa habari watawanyike mara moja.

==> Haya ni machache ambayo Nape kayaongea

1.Nia ya mkutano wangu haikuwa mbaya. Nilitaka kuzungumza na waandishi wa habari lakini Polisi wanakuja kunizuia.

2.Mnajua ni kiasi gani nimepigana kuirudisha CCM madarakani? Miezi 28 nimelala porini leo mtu anakuja kunitolea bastola.

3.Jana nilisema kuwa kuna gharama za kulipa wakati unatetea haki za watu. Na nilisema kuwa nipo tayari kuilipa gharama hiyo.

4.Sina kinyongo na serikali wala chama changu. Sikumuuliza Rais siku aliniteua na sitamlaumu kwa kuamua kuniondoa.

5.Niliikuta CCM iko shimoni nikaitoa huko. Uzalendo wangu ndani wa CCM si wa kutiliwa shaka.

6.Kina Kawawa walikuwepo wakapita, sisi tutapita, lakini tujiulize tutawaachia watoto wetu Tanzania ya namna gani?

7.Namshukuru Rais kwa mwaka mmoja alioniamini. Nampongeza kaka yangu Dkt Mwakyembe. Nawaomba mumuunge mkono Waziri Mwakyembe.

8.Nawaomba mtulie maisha yaendelee. Nape ni mdogo sana kuliko nchi. Kuna mambo mazuri mbele hivyo tuiunge mkono serikali.

9.Nilitamani sana kuendelea kufanya kazi na ninyi waandishi wa habari lakini muda wa aliyeniweka umefika akaamua niondoke.

10.Mimi niliwahi kufukuzwa CCM kwa kusimamia nilichokiamini. Ili mbegu iote na kuchanua, sharti ioze kwanza

11.Vijana naomba msimamie haki yenu

Kauli ya kwanza Ya Nape Nnauye Baada ya kutumbuliwa ...na pia kuhusu taarifa kukamatwa kwake.


Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli leo kutengua uteuzi wa Waziri  wa Habari, Sanaa, Utamaduni na michezo, Nape Nnauye....Mbunge huyo yupo hotel ya Protea tayari kwa kuongea na waandishi habari kuhusu kutumbuliwa.

Akiwa njian kuelekea Protea, silisambaa habari kwamba amekatwa. Taarifa hizo amezikanusha kupitia mtandao wa twitter na kudai yuko salama

Wanasambaza nimekamatwa! Niko njiani nakwenda Protea, niko salama nimetoka Arusha na ndege mchana huu! Nashauri waache UONGO, WATULIE!

— Nape Moses Nnauye (@Nnauye_Nape) March 23, 2017

Tukutane saa nane kamili Protea Hotel karibu na St. Peter ntakutana na Wanahabari. Karibuni sana!

— Nape Moses Nnauye (@Nnauye_Nape) March 23, 2017


Breaking News!!! Rais Magufuli afanya Mabadiliko baraza la mawaziri, Nape Nauye aondolewa Soma zaidi hapa

Rais Magufuli Leo march 23 Ametengua uteuzi wa Waziri wa Habari, utamaduni na Michezo Mh.Nape Nnauye na nafasi yake kupewa Dkt. Harrison Mwakyembe aliyekuwa Waziri wakatiba na Sheria SOMA HAPA CHINI

NAFASI ZA KAZI ZILIZOTANGAZWA LEO MARCH 23

SMS Za Nguvu Za Kutumia Baada Ya Kupewa Namba Na Mwanamke

 
Tangu tuweke chapisho ambalo linagusia swala la mbinu tofauti tofauti za kuomba namba ya simu ya mwanamke, tumekabiliwa na janga jingine ambalo baadhi wa readers humu ndani wamekuwa wakituandama katika inbox na maswali ya kurudia rudia ya 'Jinsi ya kuufunga mchezo baada ya kupewa namba na mwanamke'

Tumekuwa tukiwajibu baadhi ya readers wetu na tumeamua kuweka wazi mbinu rahisi ambayo itamfunga mwanamke ili uweze kukutana naye mara ya pili, ya tatu, ya nne...

Na kufanikisha hivi, tumekuja na mbinu ambayo kwa kawaida imekuwa ikitumiwa na guru wengi ambao wamebobea katika sekta ya kudeti wanawake.

Zama nami...Ok. Umefuata mbinu ya moja kwa moja ukamfanya mwanamke akakupatia namba yake ya simu.

Uliongea naye na uliona anavutia kupindukia...

Ulikuwa ama alikuwa na haraka hivyo hukupata nafasi ya kuongea naye kwa muda mrefu bali ulichukua namba yake ya simu.

Sahizi umeachwa hujui ufanye nini!

Je umpigie simu ama umtumie ujumbe mfupi?

Utasema ama utamwambia nini baada ya kuwasiliana naye?

Je, utamuuliza kama atoke deti na wewe au la?

Ok bila kupanic, mbinu ya kufanikisha maswali haya ni rahisi...

Mwanzo ni rahisi kama kusema A...B...C...

SMS za nguvu za kumtumia mwanamke siku ya leo baada ya kukupatia namba

1. Funga deti na yeye 
Jambo la kwanza kabisa ambalo unafaa kufanya wakati ambapo atakuachia namba yake ya simu ni uhakikishe ya kuwa unamwomba atoke deti na wewe. Na meseji unayohitajika kumtumia ni kama ifuatayo...

"Hi. nlikuwa nahakikisha kama umefika nyumbani salama. Nimefurahia sana kukutana na wewe. Ningependa tukutane wakati mwingine. Jumamosi nitakuwa free. Nije nikuchukue wakati gani?"

SMS hii huwa inafanya kazi kwa mambo mawili: Jambo na kwanza ni kuwa inamfanya ajihisi yuko salama, yani kujiona ya kuwa kuna mtu anadhamini maslahi yake, jambo ambalo wanawake wengi wanatamani kuwa nalo.

Pili ni kuwa unamlazimisha kujiazima. Aidha akubali kutoka deti na wewe ama kukukataa papo hapo. Kivyovyote vile utaujua msimamo wake.

Kama atakubaliana na wewe na kujibu sms yako,  turuke katika hatua ya pili.

2. Mfunge kwa kumpigia simu
Kabla kutoka deti na yeye lazima ufahamu mambo angalau kidogo kumhusu. Kujua mambo kadhaa kumhusu kutakupa wewe nafasi ya rahisi kuifanya deti yako na yeye kuvutia, bila kuboesha. Pia kumpigia simu kunajenga ile hisia ya mapenzi ambayo hujitokeza katika mazungumzo ya simu.

Pia unataka kumjulisha ya kuwa uko interested na yeye, lakini usiivuke mipaka yako hapa. Meseji ya pili inafaa ienda hivi:

"Poa. Natumai kukutana na wewe hio siku. Nitakupigia simu wakati flani kukujulisha vile tutavyoendelea. Kesho inaweza kuwa siku nzuri kwako?"

 Kutumia meseji hii ina nguvu zifuatazo:  Unaufunga mchezo wako wa simu. Unamwambia ya kuwa deti yenu itafanikiwa. Pia unamwambia ya kuwa unapanga sehemu ambayo unapania kukutana kwa deti. Kiukweli ni kuwa utajua vitu ambayo anapenda wakati ambapo utampigia simu, na hii itakuwa kama msingi wenu wa kwanza katika deti.

Halafu sasa itambidi akujibu. Na hapa ndipo maongezi yenu yataanza kupanda kwa kasi. Haswa kama amependezwa na wewe.

Mwanzo meseji ambazo atakuwa akituma baada ya hizi mbili kutaashiria kwako kuweza kutoka deti na yeye mara kwa mara...na hata kufanya kufikia level ya texts za kimapenzi.

Upo!?

Isome hapa ripoti nzima ya kamati iliyochunguza sakata la RC Makonda kuvamia Clouds media.


Kamati iliyoundwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuchunguza sakata la kuvamiwa kwa Ofisi za Clouds Media Group, mchana wa leo imekabidhi ripoti hiyo kwa waziri huyo huku ikisoma mbele ya waandishi wa habari kile walichokipata katika uchunguzi waliofanya.

Mmoja wa wanakamati hao akisoma ripoti hiyo katika ukumbi wa Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam alisema kuwa, kamati hiyo iliundwa ili kuchunguza sakata hilo na kuzisikiliza pande zote mbili kuhusu nini hasa kilitokea usiku wa Machi 17 katika ofisi za kituo hicho.

Kamati imeeleza kuwa baada ya kusikiliza upande wa Clouds Media Group kama alivyoeleza kwenye vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji, Ruge Mutahaba walimtafuta Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili waweze pia kusikia yeye ana kipi cha kuzungumza.

Kamati ilimtafuta Makonda kwenye simu bila mafanikio na kuamua kwenda ofisini kwake ambapo walitakiwa kusubiri nje sababu alikuwa na ugeni wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene. Aidha baada ya kumaliza maongezi yao, wanakamati waliambiwa kuwa waelekee ukumbini kuonana na RC Makonda kwa ajili ya mazungumzo.

Aidha, walipofika ukumbini hawakumkuta na walibaini kuwa alitumia mlango wa nyuma kuondoka kwa madai anakwenda katika jengo la Machinga Complex na angerudi hivyo wamsubiri. Kamati ilimsubiri kwa muda mrefu lakini walipewa taarifa kuwa kiongozi huyo amepata dharura nyingine hivyo asingeweza kurejea kwa muda ofisini kwa ajili ya mazungumzo.

Kufikia hapo, kamati ilijiridhisha pasi na shaka kuwa RC Makonda amechagua kwa hiari yake kutozungumza nao kuhusu tukio analodaiwa kulitenda la kuvamia ofisi za Clouds.

Kuhusu kama ni kweli alivamia ofisi hizo, kamati imethibitisha kuwa RC Makonda alivamia ofisi hizo usiku akiwa pamoja na Askari wenye silaha ambapo alikwenda kwa gari aliyokuwa akiendesha yeye mwenyewe na pia wamesema sababu ya kuvamia ni kutaka kurushwa kwa kipindi chake alichorekodiwa mwanamke mmoja aliyekuwa akidai kuwa amezaa na Askofu Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.

Mbali na kuwa Makonda na Askari waliokuwa na silaha waliingia katika chumba cha kurushia matangazo kinyume na sheria, lakini kamati imefafanua kuwa aliwatishia watangazaji wale kuwa angewafunga jela miezi sita au kuwataja kwenye orodha ya watuhumiwa wa dawa za kuelvya kama wasingerusha kipindi hicho. Kutokana na vitisho vingi, watangazaji hao walishindwa kufunga kipindi cha SHILAWADU katika utaratibu unaotakiwa kwani ndio walikuwa wanamalizia.

Mbali na kuwatishia watangazaji hao, Makonda aliwatisha pia wafanyakazi wengine wa Clouds Media Group kuwa yote hayo yaliyotokea yabaki kuwa siri ndani ya ofisi hiyo, na kama mtu yeyote atathubutu kuyatoa nje ya ofisi, atamjua yeye ni nani.

Kamati imejiridhisha pasi na shaka kuwa Makonda alivunja sheria ya vyombo vya habari kwa kuingia katika kituo cha habari kinyume na sheria lakini pia kujivika kazi ya uhariri wa habari ambapo yeye si mtaalamu. Lakini pia, alivunja sheria kwa kushinikiza kipindi ambacho hakijahusisha pande mbili kurushwa hewani kitu ambacho ni kinyume na maadili ya utangazaji lakini pia sheria za vyombo vya habari.

Kuhusu RC kwenda Clouds, kamati imesema ni kweli huwa anakwenda mara kwa mara na hata siku moja kabla ya kufanya maadhimisho ya mwaka mmoja wa uongozi kama Mkuu wa Mkoa, alikuwa Clouds hadi saa tisa usiku akiandaa matangazo ya maadhimisho hayo. Lakini mara zote ambazo amekuwa akienda, hakuna hata siku moja alikuwa amefuatana na Askari au kuwa na silaha.

Watangazaji waliopiga kelele usiku ule imeelezwa kuwa si kwa sababu walipigwa mtama au kupigwa na vitako vya bunduki kama baadhi ya watu wanavyodai, lakini walikuwa wamejawa na hofu kufuatia uwepo wa askari katika chumba cha kurushiwa matangazo, imeeleza kamati hiyo.

Baada ya kamati kuyasema hayo yote kutokana na uchunguzi wao, walitoa mapendekezo ambayo wanaamini yanatakiwa kufanyiwa kazi haraka.

Miongoni mwa mapendelezo yaliyotolewa ni pamoja na Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda awaombe radhi Clouds Media Group kwa tukio lililotokea lakini pia awaombe radhi waandishi wa habari wote. Lakini pia imependekezwa Waziri husika ambaye ni Nape Moses Nnauye atoe taarifa kwa mamlaka husika ili Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda achukuliwe hatua.

Pendekezo jingine ni vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi juu ya Askari kuingia katika Ofisi za Clouds Media Group kinyume na sheria tena wakiwa na silaha za moto. Na pia Clouds wameshauriwa kutazama upya sera na sheria zao ili kuzuia watu wasiohusika kuingia bila idhini na kufanya kazi za uhariri wa vipindi au kazi nyingine bila kibali cha wamiliki.

Kuhusu Waziri Nape Nnauye, amesema kuwa ripoti aliyoipokea ataiwasilisha kwa mamlaka zilizo juu yake ambao wao ndio watakaoamua juu ya hatua za kuchukuliwa dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya March 23