Header Ads

Breaking news!!!! Mbunge wa CHADEMA afariki dunia

 Dkt Elly Macha (Enzi za uhai wake)

Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Viti Maalum (CHADEMA) akiwakilisha walemavu Dkt. Elly Macha amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, ambapo amesema mbunge huyo alikuwa akipatiwa matibabu mkoani Arusha.

"Taarifa ni za kweli, mbunge Viti Maalum Dkt. Elly Macha amefariki, lakini sijapata bado taarifa za kina, lakini ninachojua ni kwamba amekuwa akipatiwa matibabu kwa muda mrefu Arusha" Amesema Makene

Miongoni mwa wabunge wa kwanza kutoa taarifa za msiba huyo ni Lazaro Nyalandu ambaye kupitia mtandao wa twitter ameandika "Mbunge mwenzetu, Mhe. Dr. Elly Macha amefariki dunia leo.

Wabunge wote tumeguswa sana na tukio hilo. Upumzike kwa amani dada yetu mpendwa"

Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitaendelea kukujia hivi punde