Header Ads

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA WAOMBAJI WA UDAHILI WA KOZI ZA ASTASHAHADA (CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA) KWA AWAMU YA MACHI/APRILI, 2017 KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

                                                 BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
                                                                                             (NACTE)

                                                                                    


TAARIFA KWA UMMA
UTEUZI WA WAOMBAJI WA UDAHILI WA KOZI ZA ASTASHAHADA (CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA)
KWA AWAMU YA MACHI/APRILI, 2017 KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi liliratibu zoezi la udahili kwa waombaji wa kozi za Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) kuanzia tarehe 23 Februari, 2017. Zoezi la maombi ya udahili lilifungwa rasmi tarehe 06 Machi 2017 ili kuruhusu uteuzi wa kwa waombaji wa kozi hizo.
Baraza linapenda kuwaarifu waombaji wa kozi za Astashahada na Stashahada; na umma kwa ujumla kuwa, matokeo kwa waliochaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali yametangazwa tangu tarehe 25 Machi 2017 kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) uliotumika kufanya maombi ya udahili. Waombaji wanashauriwa kutembelea kurasa zao (profiles) za kuombea udahili kupitia CAS ili kuona kama wamechaguliwa.
Ili kutembelea ukurasa wako, waweza pia kubofya hapa.
BONYEZA HAPA

Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
Tarehe: 26 Machi, 2017