Header Ads

Amber Lulu Aapa kutopiga Tena Picha za Utupu!


MWANAMUZIKI na video queen anayesumbua Bongo, Amber Lulu amefunguka kuwa, kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani hawezi kuthubutu kupiga picha za nusu utupu kama alivyokuwa anafanya na kwamba huo ndiyo utakuwa mwisho wake wa kupiga picha hizo.

Akichonga na Showbiz, Amber amesema ameamua kufikia maamuzi hayo baada ya watu kumsema sana mitandaoni lakini pia ingawa siyo muumini wa Dini ya Kiislamu ila ameamua kutumia mwezi Mtukufu kusahihisha makosa yake.

 “Ni kweli mapicha ya nusu utupu yananiweka mjini, lakini niyaache kwanza kupisha mwezi mtukufu wa Ramadhani, nafikiri mbali na kuupisha mwezi nitaangalia namna ya kupiga picha zangu na kuniingizia kipato kuwakacha watu wasichonge sana,” alisema Ambar Lulu.