Header Ads

TLS chini ya Lissu Kama Kweli Wanaitakia Mema Tanzania Waungane Kuzima Wizi wa Acacia

Tumesikia mengi kuhusu Acacia kutuibia Watanzania kwa kutumia mikataba, tena iliyoandaliwa na Watazania wenzetu. Kama taifa, hatuwezi kuendelea kulalamika na kunyoosheana vidole, ni lazima tuchukue hatua. Sheria sio Misahafu. Sheria zimewekwa na binadamu na zinaweza kufutwa au kurekebishwa na binadamu pia.

Pamoja na nguvu ya kifedha waliyonayo Acacia Watanzania wakiungana tutashinda hii vita ya kiuchumi. Sasa, TLS kama kweli wanaitakia mema Tanzania waungane na kusimamia mabadiliko ya sheria ili kufuta vifungu vya kinyonyaji na kuhakikisha kila kinachovunwa kwenye ardhi ya Tanzania kinalipiwa kwa haki, na sio kutumia huu ujanja wa 'commercially viable'.

Ni wazo tu
By Hekima Kwanza

Je Mdau Unaonaje Hapo?